WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI NAMABENGO WAANDAMANA

WANAFUNZI WA SHULE YA NAMABENGO SEKONDARI WAANDAMANA KUPINGA VITENDO VYA KIKATILI WANAVYOTENDEWA NA MWALIM MKUU MSAIDIZI SHULENI HAPO by JOHN BUKUKU on MARCH 1, 2016 in JAMII with NO COMMENTS Mwanafunzi wa shule ya SEKONDARI NAMABENGO ambaye hakufahamika jina akionyesha kidonda anachouguza kutokana na fimbo ambazo wanapigwa na mwalim mkuu msaidizi wa shule hiyo SHAIB CHAMPUNGA. Wanafunzi wa shule ya sekondari namabengo wakiwa wamekaa na kumsikiliza afisa elimu wa wilaya hiyo ambaye hayupo pichani . ……………………………………… Na Gidion Mwakanosya. Wanafuzi 106 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Namabengo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameandamana kwenda kumwona mkuu wa mkoa Said Mwambungu kumpelekea malalamiko dhidi ya vitendo vya udharirishaji wanavyofanyiwa na makamu mkuu wa shule hiyo Shaibu Champunga. Mwalimu huyo anadaiwa kutoa vitisho na lugha za matusi kwa wanafunzi,kuchapwa viboko visivyo na idadi,kuingi kwenye bweni la wanafunzi wa kike nyakati za usiku bila kuongozana na matroni na kuwalazimisha kutaka kufanya mapenzi pamoja na kuwazuia wanafunzi wa kike kulala bwenini. Kutokana na malalamiko ya wanafunzi hao walitaka kwenda kumwona mkuu wa mkoa ili aweze kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero zao juhudi za kutaka kuonana na mkuu huyo wa mkoa ziligonga mwamba wakati wamesha tembea kwa miguu kilomita Zaidi ya 16 kabla ya kufikla Songea mjini ambako askari polisi wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Namtumbo kuwazuia wasiendelee na maandamano. Wanafunzi hao walikutwa kijiji cha Mlete kilicho nje kidogo ya manispaa ya Songea ambapo askari polisi waliwaamuru wasimame ndipo mkuu wa polisi wilayani humo aliwataka waeleze sababbu za kufanya maandamano bila kibali,wanafunzi hao walimweleza kuwa kila mtu anahaki ya kuongea kwa kuwa walishatoa malalamiko yao kwa mkuu wa shule lakini hayakusikilizwa hivyo waliona vema wakakutane na mkuu wa mkoa labda ataasikiliza. Muda mfupi baadae alifika katibu tawala wa Namtumbo Alkwine Ndimbo na kusikiliza malalamiko mengi ya wanafunzi ambapo walimweleza kuwa makamu mkuu wa shule ya Sekondari Shaibu Champunga hawamtaki shuleni hapo kwa sababbu anatuhumiwa kuwa na lugha chafu zenye kejeri ikiwa ni pamoja na kuwataja kwa majina wanafunzi wanaodaiwa kuwa na ugonjwa wa Ukimwi. Walisisitiza kuwa shule hiyo haina miundombinu mizuri ambapo wamedai kuwa vyoo ni vibovu havifai kutumika,baadhi ya madarasa hayana sakafu paja na kwamba wanalazimika kwenda umbali mrefu kufuata maji. Baada ya viongozi hao kusikiliza malalamiko ya wanafunzi waliwataka warudi shuleni ili wakatoe maamuzi mbele ya wanafunzi wote pamoja na walimu jambo ambalo wanafunzi walikubali na kusitisha maandamano. Kwa upande wake ofisa elimu wa sekondari wilaya ya Namtumbo Patrick Atanasi ambaye aliyefika kwa kuchelewa wakati tayari katibu tawala wa wilaya hiyo Ndimbo ameshakubaliana na wanafunzi warudi shuleni alisema kuwa kitendo walichofanya wanafunzi cha kuandamana ni kosa kubwa na utovu wa nidhamu na inapaswa kilaaniwe na kuwachimba mkwara wasirudie tena jambo lililowafanya wanafunzi kuguna. Jitihaa za kumpata kamanda wa polisi ofisini kwake na kwa njia ya simu hakuzaa matunda ili kudhibitisha tukio hilo badala yake alitafutwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai moa wa Ruvuma Levokatus malimi alikili kutokea kwa tukio hilo mbalo alidai kuwa limeshaanza kufanyiwa kazi.Habari kwa hisani ya

Comments

Popular posts from this blog