TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU TANZANIA BARA MWAKA 2012/13 Jumla ya walimu 26,537 wameajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2012/13. Walimu wa ngazi ya cheti walioajiriwa ni 13,568. Kati yao walimu 13,527 wamepangwa kufanya kazi katika shule za msingi zilizopo kwenye Halmashauri na walimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Jumla ya walimu wa sekondari na vyuo vya ualimu walioajiriwa ni 12,973; wakiwemo walimu wa shahada 8,887 na wa stashahada 4,086. Walimu waliopangwa kufundisha shule za sekondari zilizo chini ya Halmashauri ni 12,893, wakufunzi wa vyuo vya ualimu ni 59 na walimu 21 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Aidha, idadi hiyo inajumuisha walimu 188 wa Elimu maalumu wenye Shahada ambao wamepangwa katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu vinavyotoa Elimu maalumu. Idadi ya walimu walioajiriwa mwaka 2012/13 imeongezeka kwa asilimia 11 sawa na walimu 2,630 ikilinganishwa na walimu 23,907 walioajiriwa mwaka uliopita 2011/12. Kati ya walimu wa sekondari na vyuo waliyoajiriwa, jumla ya walimu 1,286 (shahada 862 na stashahada 424) ni wale walioomba ajira Serikalini kutoka soko la ajira. Hawa ni tofauti na wale waliotoka vyuoni moja kwa moja. Aidha, walimu walioajiriwa ni pamoja na walimu wa ngazi ya stashahada 841 wa mwaka 2011 waliorudia mtihani mwaka 2012 na kufaulu. Kwa upande wa walimu wa elimu ya msingi, walimu 200 kati ya walioajiriwa ni waliokuwa katika soko na kuomba ajira serikalini. Naagiza kuwa walimu wahitimu ambao ni waajiriwa(inservice) wanatakiwa kurudi katika vituo vyao vya kazi walikokuwa wakifanya kazi kabla ya kwenda masomoni. Orodha ya walimu na Halmashauri walikopangwa itapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (www.moe.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa–TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz). Orodha hiyo pia itatumwa kwenye Mikoa na Halmashauri husika. Walimu wote waliopangiwa vituo vya kazi wanaagizwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri au Wakuu wa Vyuo vya Ualimu walikopangwa tarehe 1 Machi, 2013. Tarehe ya mwisho ya kuripoti ni tarehe 9 Machi 2013. Tarehe ya mwisho ya kuripoti imepangwa ili kuwezesha walimu wapya kuingizwa katika orodha ya mshahara wa mwezi Machi 2013. Watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye Halmashauri na Vyuo vya Ualimu watakuwepo kuwapokea. Walimu wote wanatakiwa kuripoti wakiwa na Vyeti vyao halisi vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, pamoja na nakala zake ili viweze kuhakikiwa na kukamilisha taratibu za ajira zao. Waajiri, yaani Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi watawalipa walimu wapya malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya Serikali kuhusu waajiriwa wapya. Nawatakia walimu wote waliopata ajiri hizi mpya utumishi mwema Serikalini katika Sekta ya Elimu. Imetolewa na: Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb) WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI 13 Februari 2013

Comments

Popular posts from this blog