TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU TANZANIA BARA MWAKA 2012/13 Jumla ya walimu 26,537 wameajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2012/13. Walimu wa ngazi ya cheti walioajiriwa ni 13,568. Kati yao walimu 13,527 wamepangwa kufanya kazi katika shule za msingi zilizopo kwenye Halmashauri na walimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Jumla ya walimu wa sekondari na vyuo vya ualimu walioajiriwa ni 12,973; wakiwemo walimu wa shahada 8,887 na wa stashahada 4,086. Walimu waliopangwa kufundisha shule za sekondari zilizo chini ya Halmashauri ni 12,893, wakufunzi wa vyuo vya ualimu ni 59 na walimu 21 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Aidha, idadi hiyo inajumuisha walimu 188 wa Elimu maalumu wenye Shahada ambao wamepangwa katika shule za sekondar...
Comments
Post a Comment